TANGAZA NASI

header ads

Zaidi ya milioni 700 zakabidhiwa kwa vikundi 72 Njombe

 



Na Amiri Kilagalila,Njombe

zaidi ya Shilingi milioni 700 zimetolewa kama mkopo kwa vikundi 72 vya kata 11 za Halmashauri ya Mji wa Njombe toka kwenye mapato yake ya Ndani kama sheria inavyoelekeza kutengwa kwa asilimia kumi ya mapato.

Enembora Lema ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya mji wa Njombe Ambaye Amesoma Taarifa ya Fedha Hizo na Kwamba Kila Mwaka Halmashauri Hiyo Imekuwa Ikitoa Mikopo Kama Sheria Inavyoelekeza.

“Fedha hizi zinatolewa kila robo kwa kutegemea makusanyo,hivyo leo utakabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni mia saba laki tisa kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”Alisema Enembora Lema kwenye taarifa yake

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya Amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe na Idara yake ya Maendeleo ya Jamii Kuhakikisha Anafuatilia Matumizi ya Fedha Hizo kama zinatumika kama Zilivyoombwa na Kutakiwa kurejeshwa ili makundi mengine Yaweze Kupata.

“Mikopo hii itumike kwa malengo yaliyokusudiwa msije mkachukua fedha hizi kama vikundi mnafika kule mnagawana kununua baiskeli na mwingine analipa ada ya watoto.Sio lengo ya mikopo hii”alisema Marwa Rubirya

“Nikuagize mkurugenzi wa halmashauri ya mji kupitia idara yako ya maendeleo ya jamii mfuatilie vikundi hivi kuhakikisha shughuli zilizolengwa kufanyika ndizo zinazofanyika”aliongeza Rubirya

Baadhi ya Wanavikundi hivyo toka kundi la wanawake,Walemavu na Vijana Deodata Mlowe,Gislaly Mwalongo na Acrey Chatanda Wameahidi Kwenda Kuzifanyia Kazi fedha hizo kadri ya Malengo yao na Kwamba Hawatazifuja kwa matumizi mengine.

 

Post a Comment

0 Comments