TANGAZA NASI

header ads

Wanawake 154 wamefanyiwa ukatili wa kimwili January - September 2020 Njombe mjini

 




Na Emmanuel Mkulu,Njombe


Takwimu zilizo tolewa mjini Njombe,kuanzia Januari hadi September mwaka huu,zinaonyesha watoto 25,walifanyiana ukatili wenyewe kwa wenyewe,huku watoto 24,walifanyiwa ukatili wa kingono na watu wazima,aidha watoto 13 walifanyiwa ukatili wa kihisia,wakati wanawake 154 walifanyiwa ukatili wa kimwili na wanawake 54 walifanyiwa ukatili wa kiuchumi. 


Hayo yamebainishwa na mratibu wa kudhibiti ukimwi,kutoka halmashauri ya mji wa Njombe,bwana Daniel Mwasongwe,katika kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia wanao fanyiwa wanawake mkoani humo,ulio andaliwa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na maswala ya wanawake UN women, ikishirikiana na Kampuni ya Chai ya Unilever chini ya mradi wa kutokomeza Ukatili wa Kijinsia katika kilimo cha zao la chai katika wilaya ya Mufindi na Mkoani Njombe ambao umeanza tarehe 6 Disemba hadi tarehe 12 Disemba mwaka huu.


Bi Yasinta Maembe ambae ni mkazi wa kijiji cha Ulenga,mkoani humo,amesema kuwa endapo mwanamke atafiwa na mwenza wake,ni ngumu sana mwanamke huyo kumiliki mali alizo acha mumewe.


"Mimi nilifiwa na mume wangu mwaka jana,nilipokonywa mashamba yote,na ndugu wa marehemu mume wangu kwa madai kuwa,sikuja na shamba kutoka kwetu nilipo olewa".


Bi Yasinta hadi sasa amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi,pamoja na kupokonywa kibanda chake cha biashara alichokuwa akimiliki enzi za uhai wa mune wake.


Ibara ya 24 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kumiliki mali na kwamba mtu huyo anayo haki ya kulindiwa mali yake kwa mujibu wa sheria.


Ila wanawake wengi wanapokonywa na kufukuzwa katika makazi yao,na hawaruhuusiwi kuziendeleza zile mali.


Ukatili wa kiuchumi ni kilio cha wanawake wengi kijijini Ulengule, mkoani Njombe.


Katika uhamasishaji wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ambo umeandaliwa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na maswala ya wanawake UN women, mkoani Njombe,limetambua mchango wa wanawake katika sekta mbali mbali za kukuza uchumi,na kutoa rai kwa jamii kupinga ukatili wa kiuchumi unao fanywa dhidi ya wanawake. 


Akiongea katika mmoja ya kongamano,meneje mradi wa kitengo cha uhamasishaji wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake,kutoka shirika hilo,bi Lucy Tesha amesema,jamii lazima itambue kuwa binadamu wote wana haki sawa.

Ameongeza kuwa endapo mwanamke atapewa pewa fursa ya kumiliki mashamba,ataweza kuleta mchango mkubwa ndani ya familia.


Mchango wa wanawake ki uchumi umeonekana kukua kwa kiasi kikubwa barani Afrika,hii imewezekana kutokana na kuondoa tofauti kati ya wanawake na wanaume. 


Dhumini la uhamasishaji huu,unao fanywa na shirika la umoja wa mataifa linalo husika na maswala ya wanawake UN women mkoani Njombe,ni kuielimisha jamii kutambua mchango wa wanawake,kupinga mfumo dume ambao upo katika jamii na kutambua kuwa wanawake wanaweza kushirikiana na wanaume kutimiza malengo ya kiuchumi.


Mtendaji wa kijiji cha Utengule,bwana Godlove Michael, amesema kuwa wanawake wengi kijijini hapo wanajishughilisha na kilimo pamoja na biashara ndogo ndogo,ila msimu wa kuvuna ukifika, baadhi ya wanaume kijijini hapo huanzisha ugomvi ndani ya familia, na kutanguli kuvuna na kuuza mazao bila kumshirikisha mwenza wake.


"Tunapokea malalamiko mengi kutoka kwa wakina mama,waliodhulumiwa haki zao,na wanawake wengi wanakuja kwetu,miezi mitatu au minne baada ya kufanyiwa ukatili huyo".


Ameongeza kuwa nguvu inabidi iongezeke katika kumlinda mwanamke,pamoja na malezi ya mtoto wa kike yanatakiwa kubadilika,kwa kumpa fursa pamoja na kipaombele mtoto wa kike.


Bwana Godlove amesema,bado jamii ina fikra potofu kuwa mtoto wa kike anapozaliwa,kazi yake ni kuolewa na kuzaa watoto,ila endapo binti huyu akijitambua na kuanza kutoa mchango wa kilimo,nguvu yake bado haitambuliwi.


Mda umefika kwa jamii kutambua nguvu kazi za mwanamke katika kukuza uchumi mkoani Njombe.


Jamii imehamasika na elimu hiyo na kuahidi kutolifumbia macho suala la ukatili pale watakapo baini wanawake wanafanyiwa ukatili

Post a Comment

0 Comments