Na Clief Mlelwa,Makambako
Wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula kanda ya Makambako,mkoani
Njombe umetakiwa kukusanya tani elfu thelethini za mazao kwa mwaka wa fedha wa 2020 /2021.
Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri wa kilimo
nchini Omary Mgumba wakati akizungumza na watumishi wa hifadhi hiyo,ambapo
amesema kuwa lengo la serikali kitaifa ni kununua na kuhifadhi mazao tani laki
tatu kwa mwaka na kanda ya Makambako inatakiwa kununua tani elfu thelathini na
kuhakikisha inapata faida katika mazao hayo.
“Malengo yetu ni kuhifadhi tani laki tatu mwaka huu
nikwasababu uwezo wetu kama NFRA ni kuhifadhi tani laki mbili na hamsini na
moja kwa sasa,lakini kwa ujenzi huu wa vihenge Makambako niliokuja kuukagua
utaongeza tani laki mbili na hamsini zingine,Kwa hiyo hapa Makambako tumewapa
tani elfu thelathini lakini hatujawapa ukomo”alisema Mgumba
Aidha Naibu waziri Mgumba amewahakikishia uwepo wa
soko la uhakika wakulima wa zao la Mahindi na Mpunga na kuwataka wasiuze mazao yote kwa sasa kwa kuwa uhitaji
wa mazao hayo ya chakula ni mkubwa
hasa nje ya nchi kutokana na mataifa mengi kukumbwa na
janga la nzige na mafuriko.
Hata hivyo kaimu meneja wa wakala wa hifadhi ya
chakula kanda ya Makambako Frank Felix amesema kuwa tani hizo elfu thelathini
zitakusanywa kwa wakati na kueleza kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni wananchi
ambao wamekua wakipeleka mahindi ambayo hayana ubora.
“Sasa hivi tunanunua mahindi na mpunga na tayari
tumeshaaanza manunuzi ya mpunga katika kituo cha Utulo ,Mbeya kwa hiyo hizo
tani thelathini ni za mahindi na mpunga,wito wangu kwa wananchi wachangmkie
hili soko”Alisema Frank Felix
Wakala wa hifadhi ya chakula kanda ya Makambako
inanunua mahindi kwa kilo moja shilingi mia tano na hamsini na mpunga shilingi
mia saba kwa kilo moja.
0 Comments