TANGAZA NASI

header ads

EWURA yakusudia kuvifungia vituo vya mafuta,vimo vya Njombe


Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji - EWURA inakusudia kumfutia leseni mfanyabiashara mkubwa wa mafuta Mansoor - MOIL na baadhi ya vituo vya mafuta kwa madai ya kushindwa kujieleza baada ya kubainika kuwa vimekiuka sheria na utaratibu wa ufanyaji biashara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam maneja uhusiano na mawasiliano EWURA Titus Kaguo amesema siku chache zilizopita ewura ilivitaka vituo hivyo kujieleza kwa nini vimekiuka sheria ambapo baada ya mchanganuo wameridhishwa na maelezo yao huku baadhi vikipewa onyo kali.


Aidha kituo cha Mtweve Oil kilichopo Chunya mkoani Songwe kimefutiwa kabisa leseni yake baada ya kubainika kuwa kinauza mafuta zaidi ya bei elekezi huku pia kikwepa kutoa risiti za kieletroniki hivyo kitatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 6 kwa EWURA ambayo itakikabidhi kwa TRA ili kiweze kulipa kodi iliyokwepwa.

Vituo vinavyokusudiwa kufungiwa ni B.O S Ways cha Bagamoyo,Mexon cha makambako,Mexon cha Njombe, huku Kampuni ya Orxy na kituo cha Mogas vikipewa onyo kali.

Post a Comment

0 Comments