TANGAZA NASI

header ads

Watuhumiwa 73,920 wa madawa ya kulevya wakamatwa kwa kipindi cha miaka mitano




Ikiwa leo ni siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kukamata Kg 188,489.93 za bangi
Jenista amesema

“Mamlaka imefanikiwa kupanua huduma za tiba kwa kuongeza vituo sita na hivyo jumla kuwa vituo nane hadi kufikia machi 2020 vikihudumia waathirika 8500 kwa siku kutoka vituo vitatu vilivyokuwa vikihudumia waathirika 3500 mwaka 2016"Waziri Jenista Mhagama.

“Katika kipindi cha miaka mitano kutoka mwaka 2015 hadi Juni, 2020, jumla ya kg 188,489.93 za bangi, kg 124,080.33 za mirungi, kg 58.46 za cocaine, na kg 635.57 za heroin, zimekamatwa pamoja na jumla ya watuhumiwa 73,920 walikamatwa"Waziri Jenista

"Mamlaka imekuwa ikisimamia upatikanaji wa uhakika wa dawa ya methadone kwa ajili ya tiba ya waraibu wa heroin kwa kusimamia uagizaji, usambazaji na udhibiti wake,kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda katika mapambano haya"Waziri Jenista

“Jamii inatakiwa kuendeleza ushirikiano wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa tatizo hili ni suala mtambuka na linahitaji ushirikiano kutoka katika taasisi za Serikali, Kiraia,Kimataifa na jamii yote kwa ujumla"-Waziri Jenista

“Mwaka 2019 tulisaini mkataba na nchi za Msumbiji na Afrika ya Kusini juu ya udhibiti wa usafirishaji wa dawa za kulevya katika njia ya kusini wafanyabiashara wengi wakubwa wamehamia katika nchi hizo baada ya udhibiti kuwa mkali nchini"Waziri Jenista

Post a Comment

0 Comments