TANGAZA NASI

header ads

Wafanyakazi wa REA watoa misaada yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa vituo vya watoto yatima na wenye ulemavu Dodoma

 


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

Menejimenti na Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini REA imetoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni kumi (10,000,000) Mkoani Dodoma ikiwa ni katika kusherekea sikukuu ya mwaka mpya.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa REA, wakati wa kukabidhi misaada hiyo katika vituo vya Miyuji kinacholea watoto yatima na wenye ulemavu na kituo cha Rahma kinacholea watoto yatima afisa uhusiano wa REA Jaina Msuya amesema wameamua kutoa misaada katika vituo hivyo ili kusherekea sikukuu ya mwaka mpya pamoja na watoto hao wenye mahitaji maalumu.

Amesema miongoni mwa vitu walivyovitoa ni vyakula, Vinywaji na vifaa vya shule vya wanafunzi ikiwamo madaftari na peni ili viweze kuwasaidia kipindi shule zitakapofunguliwa mwezi wa kwanza 2021.

" Tumeamua kutoa misaada hii ikiwa ni kuonesha kuwa tunawathamini hawa watoto pia nao washerekee sikukuu ya mwaka mpya vizuri, tumetoa vyakula vinywaji na haya madaftari yawasaidie watoto shule zitakapofunguliwa" amesema.

Mbali na misaada hiyo pia wametoa kiasi cha shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000) kwa kila kituo ili fedha hizo ziweze kuwasaidia katika kununua vitu vingine vinavyohitajika katika vituo hivyo vya kulelea watoto yatima na walemavu.

Aidha amesema REA wataendelea kushirikiana na vituo kama hivyo ikiwa ni katika kuunga mkono vituo kama hivyo na kuwafariji watoto katika vituo hivyo ili watoto nao wajione ni miongoni mwa Jamii.

Amehimiza watu binafsi, Mashirika na taasisi mbalimbali kuona haja ya kusaidia vituo kama hivyo ambavyo vinalea watoto yatima na wenye ulemavu wa viungo.

Akitoa Shukrani wakati wa zoezi hilo mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wenye ulemavu cha Miyuji, Sister Aurea Kyara ameishukuru REA kwa misaada hiyo na kubainisha kuwa itakwenda kusaidia katika malezi ya watoto pia watoto watafarijika.

Amehimiza wengine kujitokeza kuwasaidia watoto na kuona jukumu hilo ni lao  kwani watoto kama hao huhitaji upendo na kuhudumiwa misaada kama hiyo huwafariji watoto yatima na kujiona nao ni miongoni mwa Jamii.

Post a Comment

0 Comments