Na Faruku Ngonyani, Mtwara
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amezindua soko la samaki lililojengwa Kata ya Msangamkuu Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara lenye thamani ya sh. 78,458,000/= lililojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashuri hiyo.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kuzinduliwa kwa soko hilo kutatoa fursa za kibiashara kwa makundi tofauti tofauti wakiwepo Bodaboda,mama ntilie pamoja na wavuvi wenyewe kutoka katika eneo hilo .
Lakini pia Kyobya licha ya kuzindua kwa Soko hilo bado hajaridhishwa na hali ya usafi katika eneo la soko hivyo ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanafanya usafi ili liweze kuendana na mandhari ya jengo hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Thomas Luambano, ametoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya kukubali kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa Mradi wa soko hilo ambao wavuvi Zaidi ya 600 watapata fursa ya kuuza samaki wao.
Kwa upande wa mvuvi Ndg Shaibu Hamisi Kulyanganga amefurahishwa juu ya mradi huo wa soko huku akizitaja changamoto wanazokutananzo kwa sasa ikiwemo pamoja na doria zinazoendelea baharini ziwe na faida kwa wavuvi wenyewe.
Soko la samaiki la Msangamkuu litachukua wavuvi Zaidi ya 600 kutoka eneo hilo na wachuuzi Zaidi ya 30 watakaokuwa wanafanya biashara zao katika soko hilo.
0 Comments