TANGAZA NASI

header ads

Tume ya uchaguzi Uganda yatishia kumuadhibu Museveni



 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda Jaji Simon Mugenyi Byabakama, amesema kwamba tume hiyo haitasita kumchukulia hatua Rais Yoweri Museveni ambaye ni mgombea urais kupitia chama cha National Resistance Movement – NRM, endapo hatafuta sheria za kampeni zilizowekwa na tume.

Kulinana na tume ya uchaguzi, wagombea wanastahili kuandaa mikutano ya kampeni isiyozidi watu 200, na lazima wafuate maagizo ya maafisa wa afya ya kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

Maagizo hayo ni pamoja na kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Museveni amekuwa akifuata maagizo hayo na kuhutubia wafuasi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, lakini katika siku mbili zilizopita, amehutubia umati wa watu ambao hawakufuata maagizo ya afya, katika wilaya za Busia na Bukedi.

“Tutamwandikia barua kumkumbusha kwamba anastahili kufuata maagizo yetu ili sote tupambane na janga la Covid-19, maagizo yetu hayana ubaguzi na usimamizi wetu wa kampeni hauna ubaguzi” Byabakama

“Unapoidhinishwa na tume ya uchaguzi kugombea nafasi yoyote, unakuwa mgombea wetu na lazima ufuate masharti yetu,” Byabakama

“Mwelekeo tuliotoa unatumika kwa kila mgombea. Museveni ni mmoja wao na anastahili kufuata masharti yetu. Kila mgombea anastahili kuhakikisha kwamba wafuasi wake ama mawakala wake wa kampeni wanafuata masharti hayo.” Byabakama

Post a Comment

0 Comments