Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema mkoa wa Njombe amesema Chama hicho kitaendelea kusimamia msimamo wao wa
Chama wa kuto kuwatambua madiwani na wabunge waliochaguliwa kwenye nafasi zao
mpaka pale utaratibu mwingine utakapotangazwa.
Bi,Rose Mayemba ameyasema hayo wakati akizungumza na
mwandishi wetu juu ukimya wa uongozi tangu ulipomalizika uchaguzi mkuu hapo
Octoba 28 mwaka huu.
“Kama ambavyo katibu mkuu wa Chama chetu
alivyozungumza juu ya wote walioshinda kwenye nafasi zao Chama hakijabadirika
bado kwamba hawatambuliwi wabunge na hawatambuliwi madiwani, Tumezungumza na
madiwani wetu wote wa kata nne kupitia makatibu wao wa wilaya na majimbo juu ya
msimamo wa Chama na kama kuna mtu atakaidi nafikiri taratibu za Chama
zitafuatwa” alisema Rose Mayemba mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe
Aidha kuhusu ukimya wao mwenyekiti amesema ni
kutokana na sintofahamu iliyokuwa imejitokeza wakati wa Uchaguzi kwa madai ya
kugubikwa kwa vitendo visivyo kuwa vya huru na haki mpaka kutangazwa kwa
ushindi katika uchaguzi huo.
“Chadema mkoa
wa Njombe tumekuwa kimya kwa muda mrefu tangu kufanyika kwa uchaguzi kwasababu
ya sintofahamu iliyokuwa imetokea ambayo watanzania wote wanajua,Kwa muda
kidogo tulikuwa kimya kwasababu Chama kilikuwa kwenye tafakari kubwa,na
viongozi wetu wa Chama ngazi ya taifa wameshazungumza kuhusiana na uchaguzi na
sisi bado tuko imara pengine zaidi ya ilivyokuwa”Alisema Rose Mayemba
Pia ameongeza “Imani ya watanzani kwa Chadema bado
haijayumba iko pale pale katika kutafuta mabadiriko na tunaamini kila kitu
kitakuwa sawa” Rose Mayemba
0 Comments