Waziri wa mawasiliano na uchukuzi, Rahma Kassim Ali amesikitishwa na ubovu wa mashine ya meli ya MV Mapinduzi II tokea iliponunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tokea mwaka 2015.
Hayo ameyasema leowakati alipofanya ziara ya kuzitembelea taasisi zilizomo chini ya wizara yake ikiwa ni agizo kutoka kwa rais alilolitoa wakati akiwaapisha mawaziri ya kuwataka kuzifahamu taasisi na idara wanazozisimamia .
Amesema anasikitishwa na meli ya MV Mapinzuzi II kushindwa kuendelea kwa shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kwa muda wa miezi miwili sasa na kila siku meli hiyo inagharimu million nne kwa siku kwa ajili ya mafuta.
Kwa upande wa mhandisi mkuu wa meli hiyo Ramadhan Mwinyi Ramadhan amemthibitishia Waziri kuwa jambo linalopelekea meli hiyo kuharibika mara kwa mara ni kuwa meli hiyo ilinunuliwa na kukabidhiwa ikiwa na mashine mbovu.
Aidha ameutaka uongozi wa shirika la meli kuwasili wizarani kwa lengo la kukaa pamoja na kuweza kulijadili tatizo hilo ili meli hiyo iweze kufanya safari zake za Unguja na Pemba.
Pia Waziri huyo amefurahishwa na kasi ya uondoshwaji wa makontena katika bandari kuu ya Zanzibar na kumtaka mkurugenzi wa bandari Bw. Nahat Mohammed Mahfoudh kuendelea na kasi hiyo ili kuongeza mapato ya Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bandari amesema ili kuendena na kasi ya maendeleo iliyopo ipo haja kwa mamlaka ya bandari kutumia mfumo mpya wa teknolojia wa utowaji mizigo badala ya mfumo wa zamani ili kurahisisha huduma kwa watumiaji wa banadari hiyo.
Wakati huo huo waziri wa mawasiliano na uchukuzi ametoa agizo kwa wakala wa barabara kuhakikisha wanaunda kamati itakayoshughulikia ukarabatiwa barabara zote zenye mashimo kwa kuanza na barabara ya uwanja wa ndege ambayo imekuwa ikileta taswira mbaya ya mji wa Zanzibar.
Sambamba na hilo alisisitiza wafanyakazi wa wakala wa barabara kupatiwa stahiki zao wanazostahiki ili wafanyakazi hao wafanye kazi kwa ufanisi.
0 Comments