Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Wakulima na wafugaji mkoani Njombe wamesema kuanzishwa
kwa bima ya Mazao kutawafanya wakulima kufanya kilimo na ufugaji wenye tija
ambao utawafanya kupiga hatua kiuchumi.
Baadhi ya wakulima wakizungumzia hatua hiyo,mara
baada ya uzinduzi wa bima ya mazao mkoani hapa uliofanywa na serikali kwa
kushirikiana na makampuni ya kilimo pamoja na wakulima akiwemo Grace Sambala na
Frolence Tadei. Wamesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata wakati mgumu wanapokutana
na majanga kama ya ukame,mafuriko,wadudu na mengine.
“Ni majanga mengi tunayokutana nayo mfano ukame
kwa mfano mvua inaweza ikanyesha halafu ikasimama kwa kipindi kirefu .lani pia
tunaomba bima hii ije itolewa hata kwenye mifugo”alisema Grace
Awali akifafanua juu ya namna ya kujiunga na
bima hiyo ya majanga ,Mratibu wa shirika la bima la taifa-NIC Prosper Peter
anasema ni majanga ya ukame,mafuriko,mvua za mawe na mengine mengi katika
kilimo cha Mahindi na Mpunga ndio waliyoanza kutoa bima
“Mwaka 2017 serikali na taasisi zake ilikuja na mpango huu wa kuhakikisha tunatengeneza huduma ya bima ambayo itaenda kuwanufaisha wakulima pamoja na wafugaji.kwa hiyo mkulima akipata hasara ambayo inatokana na haya majanga na ikasibitika basi huyo yuko lazi kufidiwa”alisema Prosper Peter
Kwa upande wake meneja miradi wa taasisi ya TAPBDS Rahim Manji ambao ndiyo waratibu wa mafunzo kwa wakulima na mauzo ya bima pamoja na Sady Mwang'onda kutoka kampuni ya Mtewele general Traders ambao ndiyo wakala wa mikoa ya Njombe, Ruvuma wanasema ujio wa huduma hiyo unakwenda kumaliza changamoto zulizokuwa zikiwatesa kwa muda mrefu.
“Sisi kama mtewele General Traders kwa
kushirikiana na wenzetu kwa hapa Njombe pamoja na Ruvuma sisi ndio tutakuwa wasambazaji
au watoa huduma wa hii bima ya mazao”alisema Sady Mwang'onda kutoka kampuni ya
Mtewele general Traders
“Tupo kwa ajili ya
kuona umuhimu wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kwa kuwa mkulima huyu mara
nyingi akilima huwa anasubiri anaomba Mungu”alisema Rahim Manji
Bima hizo zitalipwa kwa mfumo wa vocha ambapo
vocha moja inauzwa shilingi elfu tano ikiwa na thamani ya mtaji wa shilingi
elfu 50.Aidha licha makampuni hiyo kuanza utoaji huduma hiyo ya bima lakini pia
baadhi ya maeneo mengine ya mkoa wa Njombe na Tanzania katika mazao tofauti
wameendelea kupokea huduma hiyo ya bima mazao.
0 Comments