TANGAZA NASI

header ads

Mo Dewji awapa ukweli wabunge kuhusu Bilioni 20

 


Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji amewatoa hofu wanachama na mashabiki juu uwekezaji wake wa Bilioni 20 kwakuwa mambo yakiwa sawa watafikia tamati ya mjadala huo.

Dewji ameyasema hayo Jijini Dodoma katika hafla iliyoandaliwa na wanachama wa klabu ya Simba waliopo Bungeni ambayo iliandaliwa ili kutengeneza mahusiano na wabunge wapya katika chama chao.

Katika kauli yake, Dewji amesema''Tumejipanga na tumehdamiria, Tunawaomba mtuunge mkono. Napenda kuwatoa hofu kuhusu Bilioni 20, hakuna haja ya kuwa na hofu. Simba kwangu sio biashara bali ni familia kwanza. Mapenzi yangu kwa Simba hayapimiki kwa fedha. Matamanio yangu Simba kufaniiwa kimataifa''.

Vilevile Dewji amesema malengo ya Simba yamegawanyika katika hatua tatu, kwanza ni mpango wa muda mfupi ambao ni kutetea ubingwa wa ligi kuu, malengo ya muda wa kati ni wamedhamiria kujenga klabu endelevu  huku akiainisha malengo ya muda mrefu ni kushinda ubingwa wa Afrika.

Kauli hiyo huwenda ikapunguza mijadala ambayo imeibua mashaka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kufuatia hivi karibuni muwekezaji huyo kusema kwamba Simba haina pesa na bajeti ya masuala ya uendeshaji wa baadhi ya mambo ya timu inatokana na mkono wake binafsi.

Post a Comment

0 Comments