Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea Ubunge jimbo la Wanging’ombe mkoni Njombe
Dkt Dismas Luhwago (CHADEMA) amesema kama wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza
jimbo hilo kwa miaka mitano atahakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija katika
kukuza uchumi wa jimbo hilo kwa kuanzisha mikopo ya pembejeo na kusimamia
kilimo cha mazao ya biashara yenye bei kubwa katika masoko ya kimataifa
likiwemo zao la parachichi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa
Kijiji cha Gonelamafuta kata ya kidugala ambapo amesema kuwa taarifa za
kiutafiti zinaonyesha kuwa wilaya hiyo inafursa ya kuzalisha mazao ya biashara
kama korosho,makademia na vanilla ambayo yana soko kubwa Katika masoko ya kimataifa
na bado hayajaanza kuzalishwa.
“Tutaazisha mkakati wa kulima mazao ya biashara sio
ya chakula,ya chakula mtalima kwa ajili ya chakula lakini tutakuwa na mazao ya
biashara na parachichi namba moja” Alisema Luhwago
Amesema kuwa atasimamia serikali kuwasaidia wakulima
kupata pembejeo za kilimo kwa haraka kwa
kupata mkopo kutoka bank ya kilimo.
“Serikali imeanzisha benki ya wakulima lakini kwa
bahati mbaya wananchi wengi wa Wanging’ombe mlio wengi hamna sifa ya
kukopesheka kwasababubu hamna sifa ya kukopesheka kwasababu hamna
dhamana,mashamba yenu hayajapimwa,viwanja vyenu havijapimwa.Inamaana hamna hati
tukishirikiana na serikali nitahakikisha tunapima maeneo yenu mpate hata hati
za kimila,mimi nimewahi kopa hadi miioni ishirini kwa kutumia hati za kimila”aliongeza
Luhwago
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Gonelamafuta
akiwemo Jeni Lulandala wameeleza changamoto ambazo wagombea wa vyama vya siasa
wanao omba ridhaa wanatakiwa kuzitatua.
“Kwa Kweli hata upande wa barabara tukisaidiwa
itakuwa vizuri kwasababu kipindi cha kifuku huwa tunapata shida sana”alisema
mmoja wa wananchi.
0 Comments