DODOMA
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limekamata
magari 17 yanayosadikiwa ya wizi katika maeneo tofauti ya mkoa wa Dodoma yakiwa
yamebadilishwa pleti namba pamoja na namba nyingine kwenye vioo.
Kamanda wa
polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto leo amewaambia waandishi wa habari kuwa
magari hayo yamekamatwa katika msako ulioanza Mei 19 hadi 22, 2020 yakiwa na
makosa tofauti ambayo yaliwafanya kutambua kuwa magari hayo yanasadikiwa kuwa
ya wizi.
Muroto amesema
magari hayo yamekutwa baada ya kubainika yanatumia cadi na file za magari
mengine yaliyopata ajali, yaliyokatwa chassis na kuunganishwa kwenye magari
mengine, namba za chassis kuingiliana na magari mengine, kufuta baadhi ya namba
au kuongeza au kubadilisha au kubandika vibati vya magari mengine.
Mbali ma
matukio hayo na magari jeshi la polisi linamshikilia Festo Lalika akiwa na
vifaa vya pikipiki, jenereta mbili na injini moja ya bajaji huku Lello Ringo
akimatwa na TV tatu, vifaa vya kuvunjia pamoja na panga ambapo hapa kamanda
Muroto anaeleza zaidi.
Hata hivyo
amesema ili kuifanya makoa makuu kuwa salama jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa
kushirikiana na mikoa jirani watafanya kazi kwa pamoja ili kuwadhibiti
wahalifu.
0 Comments