Na Clief Mlelwa,Makambako
Uongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe
umesema umeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho katika kata ya Utengule
halmashauri ya mji wa Makambako,kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015-2020.
Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati ya siasa ya
wilaya ya Njombe ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako HANANA
MFIKWA wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo,ambapo amesema,miradi
yote ikiwemo ya afya,miundombinu ya Barabara na umeme imetekelezwa kwa asilimia
kubwa.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kipindi
cha miaka mitano afisa mtendaji wa kata ya Utengule MOSSES MWALONGO kwa niaba
ya diwani amesema kuwa kata hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali
ikiwemo ya Elimu msingi na Sekondari.
Naye diwani wa kata ya Utengule STEPHANO MGOBA
amesema amefanikiwa kutekeleza miradi hiyo kutokana na kuwashirikisha wananchi
na kueleza kuwa katika kipindi hicho cha miaka mitano ametumia fedha zake
binafsi zaidi ya milioni 20 kuwawezesha wananchi katika shughuli zao.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata hiyo
wameridhishwa na utendaji kazi wa diwani huyo kwa kipindi hicho cha miaka
mitano.
0 Comments