Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mtungi, amevikumbusha vyama vya siasa kukabidhi ratiba zake za mchakato wa mambo mbalimbali wanapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Amesema
kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa vinapaswa kumshirikisha Msajili
kwenye ratiba zao ndani ya vyama kuhusu mchakato wa uchaguzi.
Amesema
hadi sasa hakuna mabadiliko ya Uchaguzi Mkuu na kwamba licha ya uwapo
wa ugonjwa wa corona, shughuli zitaendelea kama kawaida, lakini kwa
tahadhari kubwa.
“Tulishawaandikia kwa mujibu wa sheria ya vyama vikifikia kwenye mchakato wa uchaguzi wakumbuke kutupatia ratiba zao
“Hatuvizii
ili wakosee bali tunawakumbusha mapema kuweka wazi ratiba zao ili nasi
tushiriki…wakienda kinyume tumepewa nguvu kisheria kuweka pingamizi,”
alibainisha.
Hivi
karibuni, vyama vya CCM, Chadema na ACT Wazalendo, vilitangaza kuanza
michakato ya ndani kuelekea uchaguzi mkuu ambao umebakisha miezi mitano
Majukumu
ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusajili chama cha siasa
kinachokidhi vigezo vya usajili kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa
ya mwaka 1992, ikiwamo kufuta chama chenye usajili wa muda au kudumu
ambacho kwa mujibu wa sheria kimepoteza sifa ya usajili.
0 Comments