Na Amiri kilagalila,Njombe
Wananchi wa vijiji vya kata ya Itulahumba
halmashauri ya wilaya ya Wangingombe mkoani Njombe kwa pamoja wamepinga kitendo
kinachofanywa na baadhi ya wananchi wenzao kwa kushirikiana na mtendaji wa
kijiji hicho kuuza eneo ambalo limetengwa kijijini hapo kwaajili ya ufugaji na
kilimo.
Eneo hilo lenye ukubwa wa zaidi ekari 80 ambalo
limeanza kukatwa miti na kulimwa bila makubaliano ya kamati za vijiji pamoja na
mkutano wa hadhara wa wananchi Hao Akiwemo Yohana Mgute na Mary Mwakajuba
wamesema serikali isaidie waliovamia kukamatwa na kuzuia uharibifu unaoendelea.
“Eneo hili lirudi serikalini bila kujali kuna watu
wamepata visenti kwa kuuza sisi tunataka eneo lirudi”alisema Yohana Mgute
Mtendaji wa kijiji hicho Rudlof Mbilo anasema eneo
hilo licha ya kuwa limetengwa kwajili ya shughuli za kilimo na ufugaji
lakini hakuna nyaraka zinazothibitisha
na ndio sababu amekuwa akiidhinisha watu kuuziana ardhi hiyo.
“Hizo ekari tano zilizoanzwa kuuzwa alionwa
mwenyekiti wa kijiji pamoja na mimi huku mmuzaji akihitaji kuuza ekari kumi”alisema
Rudlof Mbilo
Viongozi wa kata hiyo wakiongozwa na diwani Thobias
Mkane na Betty Mangula Afisa Mtendaji wa Kata Hiyo wamepiga marufuku mtu yeyote kufanya shughuli katika eneo hilo
wakati uchunguzi wa kuwabaini waliovamia na kuuza ukiendelea.
“Sasa
tunasimamisha eneo lile lisiendelee kutumika tena,sisi tunayefahamu hapa
tumepokea madaraka mpaka mara tatu lakini hatujaona mtu akiishi mle,kwa hiyo
liachwe kutumika mpaka ufumbuzi utakapopatikana”Alisema Thobias Mkane
0 Comments