Na Amiri Kilagalila,Njombe
Serikali imetangaza kuanzishwa kwa kituo cha kununua
mazao ya mahindi wilayani Ludewa mkoani Njombe,kutokana na changamoto kubwa
iliyokuwa ikiwakumba wakulima wa zao hilo pindi wanapohitaji kuuza mazao yao.
Makama wa Rais ambaye pia ni mgombea mwenza wa jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mpainduzi.Akizungumza na wananchi wa Mlangali
kwenye mkutano wa kuomba kura amesema kutokana na changamoto ya Soko ndani ya
wilaya ya Ludewa amezungumza na wakala wa Taifa wahifadhi wa Chakula (NFRA)
ambao wameahidi kuanzisha kituo cha kununua zao la mahindi wilayani humo.
“Nikiwa Ludewa nilisikia kuna changamoto ya soko
kwenye mazao ya chakula,Niwape habari njema kuwa kuanzia wiki ijayo haitazidi
Ijumaa NFRA watakuwa hapa wameanzisha kituo cha kununulia mahindi” alisema Samia
Suluhu Hassan
Vile vile katika sekta ya elimu,mgombea mweza
amezungumzia kuhusu ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA) chama mkoa wa Njombe
kinachojengwa wilayani Ludewa.
“Ndani ya wilaya hii ya Ludewa pale
Shaurimoyo,serikali inajenga chuo cha ufundi Veta lakini kilisimama kwa muda
kwasababu ya uzembe wa mkandarasi na sasa serikali imeingilia kati tumeondo
mkandarasi mzembe”alisema Samia Suluhu Hassan Mgombea mwenza wa Urais JMT
kupitia CCM
Aidha amesema “Tumeita tenda wakandarasi wengine wameomba
na punde watarudi kumalizia chuo cha ufundi pale Shaurimoyo” aliongeza Samia
Suluhu Hassan Mgombea mwenza wa Urais
Naye mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Ludewa Mh,Joseph
Kamonga amewatia moyo wananchi wa Ludewa juu ya serikali kukamilisha ujenzi wa
chuo cha ufundi huku akiishukuru serikali kuonyesha nia ya kukamilisha ujenzi
“Ludewa tumependelewa sana.Serikali imeonyesha nia
ya kukamilisha Chuo cha VETA Shaurimoyo ili vijana watakaopewa ujuzi wa aina
mbali mbali pale waweze kuajiliwa kwenye viwanda ikiwemo Mchuchuma na Liganga” alisema
Joseph Kamonga
Baadhi ya wananchi wa Mlangali wanasema kujengwa kwa
chuo cha ufundi kwenye wilaya yao kutasadia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata
ujuzi mbali mbali utakao wawezesha kupata ujuzi.
0 Comments