Na Amiri Kilagalila,Njombe

 

Mgombea ubunge jimbo la Ludewa mkoani Njombe kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM wakili Joseph Kamonga,ametaja vipaumbele tisa atakavyovisimamia na kuvitekeleza endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu oktoba 28 mwaka huu.

 

Kamonga amevitaja vipaumbele hivyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za jimbo la Ludewa uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Itundu kata ya Mlangali uliohudhuriwa na viongozi wa chama mkoa na wilaya ya Ludewa na kuvitaja vipaumbele hivyo  kuwa  ni,madini,miundombinu,afya,kilimo,mifugo,uvuvi,ajira kwa vijana na elimu.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Kamonga amesema atawatumikia wananchi wote bila kubagua na kwamba atakwenda kuisumbua serikali kuhusu mradi wa makaa ya mawe ya Liganga ambayo ni hazina kubwa kwa taifa na wananchi wa Ludewa.

 

‘’Uthamini ulifanyika mwaka 2015,fidia bado hazijalipwa kwa hiyo nitajitahidi sana kuisumbua serikali kwanza kuhakikisha fidia zinalipwa,unajua miradi haijaanza kutokana na uzalendo wa jemedari wetu dkt John pombe Magufuli alivyoona ule mkataba auna maslahi kwa wananchi wa Ludewa ndo maana tunaona miradi imechelewa’’alisema.

 

Aliongeza kuwa”Lakini kwa uzalendo wake huo sisi tutakwenda kumuomba aweze kulipa fidia wananchi wale kwa sababu zile ni takribani bilioni 12,ebu mniambie jamani bilioni 12 zikimwagika Ludewa si tutabadilika sana,kwa hiyo nitafuatilia wale wananchi badla ya kuwazuiya kufanya shughuli zao za kiuchumi na uzalishaji mali waweze kulipwa fidia ili waache yale maeneo mikononi mwa serikali’’alisema,

 

Hata hivyo Kamonga alisema kuwa”lakini na sisi pia wanaludewa tuweze kugaiwa vitalu tufanye uchimbaji mdogo mdogo wa  yale madini ambayo yanakubalika hiyo itakua inatoa ajira kwetu na tutapongeza kipato’’alisema.

 

Aidha Kamonga alisema jambo jengine ni kuhusu ujenzi wa chuo cha ufundi stadi VETA Shaurimoyo kuhakikisha kinakamilishwa ili vijana wa Ludewa waweze kusoma na kupata ujuzi mbalimbali ambao utawasaidia kupata ajira.

 

‘’Najua Ludewa inavijana wengi ambao hawana ajira nilikua napitia ilani ya chama cha mampinduzi CCM nimeona mambo mazuri kuna mkakati wa kusaidia vijana,wanawake na makundi maalumu ile mikopo tunakwenda kuhakikisha itolewa,vikundi mbalimbali vinaundwa na kuhimarisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwa vijana,wakinamama na hata wazee’’alisema Kamonga.

 

Naye Mgeni rasmi katika uzinduzi huo mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC kutoka mkoa wa Njombe Fidelis Lumato,aliwataka wananchi wa Ludewa kuchagua tena Rais,wabunge na madiwani wa chama hicho kwa miaka mitano ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.

 

Kwa upande wa mgombea nafasi ya udiwani kata ya Mlangali kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Hamis Kayombo,alisema kuwa kwa maslahi ya kata hiyo wamchague kwa kumpa kura nyingi na hivyo wasiadaike na vyama vya  upinzani.

 

Katika uzinduzi huo wanachama wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA kata ya Mlangali wapatao 27 wamekihama chama hicho na kutimkia chama cha mapinduzi CCM.