TANGAZA NASI

header ads

Waziri Jafo aweke jiwe la msingi soko jipya mkoani Njombe,akabidhi hundi yenye zaidi ya Bilioni tano




 Na Maiko Luoga Njombe
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe, Seleman Jafo Agosti 17/2020 ameweka jiwe la msingi katika Soko jipya na la kisasa  lililojengwa Mkoani Njombe ambalo kwa sasa limefikia asilimia tisini na saba za utekelezaji.

Baada ya kukamilika Soko hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa zaidi ya wafanyabiashara mia saba huku likikadiriwa kuongeza makusanyo ya mapato ya Halmashauri hadi kufikia millioni mia tatu kwa mwaka tofauti na soko la awali ambalo lilikuwa likikusanya wastani wa shillingi Million hamsini kwa mwaka.

Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi kwenye Soko hilo litakalogharimu  Fedha za Kitanzania kiasi cha Shilingi Billion 10.5  hadi kukamilika kwake pia Waziri Jafo amefanya uzinduzi wa mpango kabambe  wa matumizi ya Ardhi  (Master Plan) katika Halmashauri  ya Mji wa Njombe.

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa Mzee Jassel Mwamwala walishiriki Tukio hilo na kushuhudia utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt, John Pombe Magufuli.

Katika Hatua nyingine MHE, Jafo amekabidhi mfano wa hundi ya Makusanyo ya Madeni sugu ya iliyokuwa Benki ya NJOCOBA, SACOSS na AMCOS yenye zaidi ya Fedha za Kitanzania kiasi cha Shilingi Bilioni tano.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mfano wa hundi hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe  Bi, Catalina  Revocati alisema fedha hizo zimekusanywa na kikosi kazi kulichoundwa Oktoba 23/2019 na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe, Christopher Ole Sendeka.

Mbele  ya wakazi wa Mkoa wa Njombe walioshiriki tukio hilo Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbung’o alisema wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais ya kukusanya fedha kwa wadaiwa wote Nchini ili fedha hizo zirejeshwe kwa Wananchi.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo pamoja na Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Bw, Charles Malunde wametoa onyo kwa Watendaji  wanaohusika na ukusanyaji wa Fedha hizo kuhakikisha zinarejeshwa na kuwanufaisha walengwa.

Post a Comment

0 Comments