TANGAZA NASI

header ads

Maduka kuendesha biashara kwa zamu Rwanda ili kudhibiti corona



Masoko kama hili ni mojawapo ya maeneo ambayo yamepatikana na maambukizi mapya ya coronaImage caption: Masoko kama hili ni mojawapo ya maeneo ambayo yamepatikana na maambukizi mapya ya corona

Masoko na majumba makubwa ya biashara katika mji mkuu wa Kigali Rwanda yameagizwa kuendesha biashara kwa kiwango cha 50% huku yakipokezana, kama mojawapo ya hatua mpya za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Agizo hilo lililoidhinishwa na kikao cha baraza la mawaziri limekuja kufuatia kupanda zaidi kwa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya corona kwa siku hivi karibuni.

Visa vipya vya watu waliopata maambukizi imefikia karibu 1000 katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Maduka yatatakuwa kuendesha biashara kwa awamuImage caption: Maduka yatatakuwa kuendesha biashara kwa awamu

Wengi kati ya watu waliopata maambukizi walikuwa ni kutoka kwenye masoko ya mji mkuu Kigali.

Usafiri wa umma kati ya mji mkuu na mikoa mingine umezuiwa, hukumarufuku ya kutotembea usiku kote nchini ikiendelea kati ya saa moja jioni na saa kumi na moja alfajiri.

Watu wengi wamekuwa wakipelekwa kukaa usiku kucha kwenye viwanja vya michezo kwa kukiuka marufuku hiyo baada ya saa tatu usiku.

Hadi sasa Rwanda imerekodi visa 3,625 vya Covid-19 na vifo ni 15. 

Post a Comment

0 Comments