Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katibu mkuu ofisi ya Rais Dokta Moses Kusiluka
ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya uongozi wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) amewaonya watakaosababisha kuwepo kwa kaya
hewa zinazonufaika na mpango huo awamu ya tatu baada ya kukamilika kwa uhakiki
unaofanyika nchi nzima.
Dokta Kusiluka ametoa onyo hilo alipozulu mkoani Njombe
katika mtaa wa Uwemba na kuzungumza na walengwa wa TASAF wakati wa zoezi la
uhakiki likiendelea na kwamba mkono wa
sheria hautamuacha yeyote atakayehusika kuingia katika mpango huo ilihali hana
sifa.
“Kwa hiyo ikitokea kiongozi amefanya hivyo,hatua za
kisheria zitachukuliwa kwasababu ni ubadhilifu na hatua zitachukuliwa kwa
kiongozi na muhusika anayekuja kuchukuwa fedha,hayo ni maelekezo ya Mh,Rais”alisema
Dokta Moses Kusiluka
Baadhi ya walengwa wa TASAF katika mtaa wa Uwemba
mkoani Njombe akiwemo Ostakia Ndawala na
Selina Nyakalua wanakiri kuwa TASAF imewasaidia sana kwenye mambo ambayo walikuwa
hawawezi kushughulikia kama kuwapeleka watoto shule na hata kuendeleza shughuli
za ufugaji.
“Tulikuwa maskini sana lakini tulipopewa zile hela
tayari uwemba tunakula parachichi,tuna kuku na sasa hivi tunaendelea
vizuri,mkampe salam sana Rais kwa kutukumbuka kwenye mradi huu, na sisi tuko
nyuma yake na safari hii tunataka apite tena” Alisema Selina Nyakalua
Selestin Mwanyika ni mwenyekiti wa mtaa wa Uwemba anasema
awamu moja ya uhaulishaji fedha walizopata walengwa katika mtaa wake zimeonesha
mafanikio makubwa huku akiwataka endapo watapata fedha nyingine baada ya
uhakiki wazielekeze katika malengo mahususi.
“Tangia naingia madarakani wamepata mara moja na
sikuona matatizo yoyote,lakini tuliona mafanikio wengi wamefuga kuku,na wengine
wamefuga nguluwe japo kwenye Nguruwe huku kuna myumbo” alisema Selestin Mwanyika
Jumla ya wanufaika 132 wa TASAF katika mtaa wa Uwemba wameendelea kuhakikiwa
ili kujiridhisha kama wana sifa zinazohitajika katika mpango huo lengo la
serikali likiwa ni kutaka kuondoa kaya hewa ili zisalie kaya sahihi katika
mradi.
0 Comments