Mwanaharakati maarufu anaepigania demokrasia Hong Kong, Nathan Law, ameukimbia mji huo na kwenda katika eneo lisilojulikana, baada ya kutoa ushahidi mbele ya wabunge wa Marekani dhidi ya sheria kali ya usalama iliyotangazwa na China ambayo inapunguza kwa kiasi kikubwa haki ya kiraia ya wakazi wa Hong Kong.
Law ameondoka Hong Kong siku mbili baada ya sheria ya usalama wa kitaifa kuanza kutekelezwa. Sheria hiyo inawalenga wale wanaotaka kujitenga, vitendo vya kichochezi na kigaidi, pamoja na vikosi vya kigeni vinavyoingilia masuala ya ndani ya Hong Kong.
Polisi iliwakamata watu wapatao 370 hapo juzi, 10 kati yao wameshikiliwa kwa tuhuma za kukiuka sheria hiyo ya usalama wa kitaifa, kufuatia maandamano ya kuipinga sheria hiyo.
0 Comments