TANGAZA NASI

header ads

Saba Saba kuvutia wawekezaji Yanga

Yanga Sports Club For Life - Naipenda yanga - Posts | Facebook

Yanga imesema imesema inayatumia maonyesho ya Saba Saba kujitangaza zaidi na kuwavutia wawekezaji.
Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga,umesema maonyesho ya kimataifa ya biashara ya arobaini na nne ya Saba Saba yanayofanyika nchini Tanzania,ni moja ya sehemu ambayo wataitumia kuwavutia wawekezaji na wafanyabiashara ambao watawatumia kukamilisha miradi waliyonayo hivi sasa.

Hayo yamesemwa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa mabingwa hao wa kihistoria katika ligi kuu ya Tanzania bara,Hassan Bumbuli katika viwanja vya Saba Saba vilivyopo  Temeke jijini Dar es salaam.

Bumbuli amesema kuwa kupitia maonyesho hayo yanawapa fursa wao kukutana na watu na makampuni mbali mbali na kuwaelezea juu ya bidhaa na miradi waliyonayo ambao bila shaka yatawasaidia kupata usaidizi wa kuikamilisha mipango yao.

Vilevile Bumbuli amesema kwamba wamepanga kufanya usajili wa wanachama wapya jambo ambalo lina mpango la kukusanya takwimu za wanachama wao na huo ni katika mpango wa kuelekea kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa kisasa wa timu yao.

Wanachama na washabiki wa Yanga wamesisitizwa kujitokeza katika maonyesho hayo ili wapate fursa ya kukutana na wachezaji wao ambao hawajasafiri na timu kuelekea kanda ya ziwa.

Post a Comment

0 Comments