Dodoma. Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru) Brigadia Jenerali John Mbungo amewasimamisha kazi watumishi wote tisa wa kitengo cha usimamizi wa miliki Takukuru ambao walihusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo saba ya taasisi hiyo.
Pia amekivunja kitengo hicho pamoja na kuunda tume huru ya watu wanne kutoka nje ya Takukuru itakayochunguza majengo hayo ikiwa ni pamoja na kujua kama kuna wizi, rushwa pamjoa na ubadhirifu kwa muda wa siku saba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa Mbungo amesema uamuzi huyo ni utekelezaji wa maelekezo na maagizo yaliyotolewa na Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya taasisi hiyo wilaya ya Chamwino mkoani hapa.
Jana wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo Rais Magufuli alizungumzia majengo saba ya taasisi hiyo yaliyopo katika wilaya mbalimbali ambapo hata hivyo alisema majengo mengine hatayazindua badala yake akawaagiza baadhi ya viongozi kuzindua majengo hayo.
Rais Magufuli alisema kiwango cha fedha kilichotumika katika ujenzi wa majenego hayo hakilingani na thamani ya maengo husika (hakuna volue for money).
Majengo mangine ni katika wilaya ya Mpwapwa, wilaya ya Ngorongoro, wilaya ya Manyoni, wilaya ya Masasi, wilaya ya Namtumbo pamoja na lililopo wilaya ya Ruangwa, ambapo haoa mkurugenzi mkuu wa Takukuru analeza kuhusu waliosimamishwa kazi.
Akizungumzia kuhusu tume huru aliyoiunda, Mbungo amesema tume hiyo ina watu wanne na wanatakiwa kufanya uchunguzi katika majengo hayo iwapo kuna ubadhirifu, wizi au rushwa zilizotumika katika ujenzi huo.
Mbungo amesema tuhuma zozote zitakazothibitika zitachukuliwa hatua kali za kisheria.
0 Comments