Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage ametangaza ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwa nafasi za urais, ubunge na udiwani ambapo kwa nafasi ya urais fomu zitaanza kutolewa Agosti 5 hadi 25, 2020 jijini Dodoma.
Fomu za kuwaniaa ubunge na udiwani zitatolewa Agosti 12 – 25 katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi za halmashauri za wilaya na makao makuu ya kata.
0 Comments