Na Omary Mngindo, Bagamoyo
Julai 22
WAJUMBE 480 waliopiga kura za maoni nafasi ya Ubunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Jumanne ya Julai 21 wamempigia kura za ndio 157 Mwarami Mkenge kwenye nafasi hiyo.
Kinyang'anyiro hicho kilichokuwa chini ya Msimamizi Gullamhussein Kifu (Mkuu wa Wilaya ya Kibiti), wapigakura hao walikuwa na kazi ya ziada kuwapigia kura wagombea 51, mkutano ukihudhuliwa na Kamati ya siasa wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa Abdul Sharifu.
Mkenge aliyejinyakulia kura 157 dhidi watiania wenzake Shukuru Kawambwa aliyepata kura 90, Abdul Buheti 60 huku Aboubakary Mlawa akijipatia kura 50 wakati waliosalia wakipata kura chini ya kumi, wakati zilizoharibika zikiwa 2.
Zoezi hilo lililorudiwa mara mbili baada ya kubainika ongezeko la kura 49 zaidi ya idadi halisi, lilitokea baada ya msimamizi Kifu akishirikiana na wajumbe wakihusishwa wagombea kuanza kujiridhisha karatasi zilizopigwa, kabla ya kuhesabiwa ndipo ikabainika ongezeko hilo.
Baada ya tukio hilo lililoleta maoni tofauti kutoka kwa wajumbe, ambapo kati yao walitaka zoezi liahirishwe ili lipangiwe siku, huku wengine wakisema limalizike hapohapo, ndipo Kifu alipompatia nafasi Subira Mgalu aliyesema kuwa wenye mamlaka ga kuusogeza mbele in viongozi wa CCM Taifa, huku akitaka uhakiki wa wajumbe kujua walioondoka.
"Kanuni za chama chetu kinasema kuwa mwenye mamlaka ya kuahirisha zoezi la upigaji wa kura ni viongozi ngazi za juu na si wajumbe wa mkutano wanaopiga kura, niwaombe tutulie tuwasikilize viongozi ili zoezi limalizike badala ya maoni yenu ya kutaka kuaihishwa," alisema Mgalu.
Baada ya Mgalu akapewa nafasi Dkt. Shukuru Kawambwa aliyesema kuwa ili kutofanyika makosa mengine kura zipigwe kwa kuwekwa enye boksi la kila Kata, kisha kuhakikiwa baada ya hapo ziwekwe kwenye boksi moja, hatua itayowezesha kupatikana kwa idadi sahihi ya kura kulingana na idadi ya wajumbe.
Baada ha ushauri huo ulioungwa mkono na wajumbe wengi hatimae zoezi la upigaji kura awamu ya pili likaanza kabla ya kumalizika saa 4.45 usiku, kabla ya kutangazwa matokeo ambapo kabla ya zoezi hilo Kifu iwasihi wajumbe kutoshangilia zaidi ya kupiga makofi ya kupongeza watakapotangazwa na kura zao.
Akihitimisha zoezi hilo, Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa Sharifu aliwasihi wanachama hao hususani viongozi kuzingatia kanuni zinazokiongoza chama chao, wakati wakielekea kwenye kura za maoni nafasi za Udiwani linalotaraji kufanyika hivi karibuni.
0 Comments