Na
Amiri Kiligalila,Njombe
Mkuu
wa mkoa wa mpya wa Njombe Eng,Marwa Mwita Rubirya aliyeteuliwa na kuapishwa
hivi karibuni na Rais John Pombe Magufuli , amewasili kituo cha kazi na
kuzungumza na baadhi ya watumishi wa mkoa na wilaya ya Njombe ambapo amesema
atafanya ziara katika wilaya zote nne za mkoa wa Njombe huku akiomba
ushirikiano kwa viongozi wa wilaya hizo.
Mara
baada ya kuwasili katika ofisi za mkoa ,mkuu huyo mpya amepokea taarifa kutoka
kwa katibu tawala wa mkoa wa Njombe Bi,Catarina Revocat na mkuu wa wilaya
ya Njombe Ruth Msafiri muda mfupi baada ya kukaribishwa.
“Wananchi
wa Njombe ni wananchi wasikivu,wachapakazi na tunaamini utafanya nao kazi
vizuri sana”alisema Catrina Revocat katibu tawala wa mkoa wa Njombe
Eng
,Marwa Mwita Rubirya ameahidi kushirikiana na viongozi wa halmashauri
mkoa na wilaya katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi vijijini.
“Nitategemea
ushirikiano mkubwa kwa wenzangu hapa na ambao wako wilayani,najua taarifa itaandaliwa
ili inisaidie kujifunza Njombe tunafanya
nini na ni wapi tuongeze nguvu zaidi ili hatimaye tuwasaidie wananchi”alisema Eng
,Marwa Mwita Rubirya
Rubirya
awali alikuwa meneja wakala wa barabara Tanzania (TANROD) mkoa wa Mwanza na amechukuwa nafasi
ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka aliyekwenda kwenye majukumu mengine ya kisiasa.
0 Comments