Na
Jackline kuwanda
Mkuu wa wilaya ya
chemba Mh Saimon Odunga amesema katika kuendelea kuimarisha kilimo cha
umwagiliaji kwa wakulima,serikali imefanya jitihada ya kuwapelekea umeme
wa gridi ili kuendesha mitambo ya umwagiliaji.
Akizungumza
na kituo hiki amesema pamoja na kupeleka umeme huo bado wakulima wanachangia
fedha nyingi na kusababisha gharama kuwa kubwa hivyo wanafanya jitihada
kupitia wadhamini ili kununua solar zitakazosaidia kupunguza gharama hizo.
Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo inafanya jitihada kupata
umeme wa upepo na kuachana na matumizi ya umeme wa gridi kwa wakulima wa kilimo
cha umwagiliaji walayani humo.
Odunga amesema Kilimo cha umwagiliaji kimechangia mwamko
mkubwa kwa wakulima licha ya hivi karibuni kuwepo kwa changamoto nguvu ya
kuendesha mitambo.
Katika
kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kina kuwa na tija kwa wakulima Halmashauri
hiyo imeweka vikundi vya vijana ambao wamepewa mkopo wa kulima mashamba
ya umwagiliaji ili kujiingiza kipato.
0 Comments