Na Jackline kuwanda,
DAR ES SALAAM
Waandishi wa Habari
wanawake wameshauriwa kuwa na hali ya kujiamini katika majukumu yao ya kazi
huku wakisisitizwa kuzingatia Sheria,kanuni,Taratibu, Misingi na Taaaluma ya
kazi yao.
Pia wameshauriwa
Kufuata Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari hasa katika kipindi hiki ambacho
nchi inaelekea katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es salaam na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo
Lilian Shirima wakati akifungua semina ya Kitaifa ya Wanawake Wanahabari
kwaajili ya kukuza fani yao pamoja na Kubadilishana uzoefu.
Ameendelea kusema kuwa
wanawake wanahabari wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika kazi zao
ikiwemo manyanyaso katika vyombo vya habari hivyo amewaaswa wanawake kuendelea
kujiamini zaidi hasa kwa kile ambacho wamekuwa wakikifanya katika majukumu yao
ya kazi.
Akizungumzia lengo la
semina hiyo ,Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi Rose Reuben amesema wamelenga
waandishi wa Habari Wanawake Vijana kwaajili ya kuwajengea uwezo wa kuhimili
changamoto ambazo ziko katika taaluma ya Habari.
Mwanahabari Mkongwe
Rose Mwalimu ambaye ndiye alikuwa mwezeshaji katika semina hiyo na
akizungumzia umuhimu wa vyombo vya Habari katika kuleta usawa wa kijinsia
amesema usawa wa jinsia unahusishwa kwa undani maendeleo endelevu ambayo
ni muhimu kwa utambuzi wa haki za binadamu kwa wote.
0 Comments