TANGAZA NASI

header ads

Waziri Jafo atoa maagizo kwa ma RC,DC


 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo amewaagiza wakuu wa wilaya na mikoa hapa nchini kuhakikisha wanatumia vifaa vilivyotengenezwa na viwanda vya ndani.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo amewaagiza wakuu wa wilaya na mikoa hapa nchini kuhakikisha wanatumia vifaa vilivyotengenezwa na viwanda vya ndani ya nchi katika miradi mbali mbali ya ujenzi wa miundo mbinu ya zahanati shule na hospitali ili kulinda viwanda hivyo ambavyo vimekuwa vikizalisha bidhaa zenye ubora. 
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati alipifanya ziara ya kukitembelea kiwanda cha Africab kilichopo katika wilaya ya Temeke.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amesema atahakikisha analisimamia agizo hilo la Mh Jafo kwa kuwa kufanya hivyo pia kunalenga kulinda katika viwanda hivyo.
"Ni kweli viwanda hivi vinatumia malighafi zenye viwango na kuzalisha bidhaa za matumizi ya ndani na nje kutoa nafasi kwa viwanda vya ndani vitasaidia kukuza uchumi wa nchi" amesema Gondwe

Post a Comment

0 Comments