TANGAZA NASI

header ads

Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) inatarajia kuwa kitovu cha upandikizaji wa figo Afrika Mashariki





DODOMA.

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa (BMH) inatarajia kuwa kitovu cha upandikizaji wa figo Afrika Mashariki kwa kutumia wataalam wa ndani inayochagizwa na maendeleo katika sekta mbalimbali chini ya serikali ya awamu ya Tano.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Jijini Dodoma Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dr Alphonce Chandika amesema  wamefanikiwa kupandikiza figo kwa mgonjwa mwingine tangu walipofanikiwa kufanya hivyo kwa mgonjwa wa kwanza 2018 na kufanya mgonjwa huyo kuwa wa pili kwa kutumia wataalam wa ndani.

Dk.chandika amewaasa watanzania kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara badala ya kusubiri kuwa na Hali mbaya ndipo wafike hospitali kupatiwa huduma na kuongeza kuwa  jumla ya wagonjwa 75 wanaendelea kupatiwa huduma ya matibabu ikiwemo usafishwaji wa figo katika hospitali hiyo .
  
Kwa upande wake, mganga mbobezi wa magonjwa ya Figo, katika hospitali hiyo, Keissy Shija, amesema , huduma hizo za upandikizaji na usafishaji wa figo zitakuwa endelevu na zitakuwa huduma za kawaida za kila siku kama nyingine.
  
Profesa. Ipyana Mwampagatwa, Akizungumza kwa niaba ya Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM), amesema, waliweka malengo ya miaka mitano kuanza kutoa huduma hiyo kwa kutumia wataalam wa ndani lakini ndani ya miaka miwili wameweza kukufanikisha hilo, ni hatua kubwa sana ambalo lilihitaji udhubutu.

Mwampagatwa, ametoa  wito kwa BMH, kuongeza juhudi katika eneo hilo ili waweze kusaidia kusambaza ujuzi katika hospitali nyingine ndani ya Tanzania na afrika Mashariki kwa ujumla.



Post a Comment

0 Comments