Na Amiri Kilagalila,Njombe
Zoezi la uhakiki wa kaya zinazonufaika na mpango wa
maendeleo ya jamii TASAF limeanza
kufanyika mkoani Njombe na walengwa wakikiri mradi huo kuwa msaada mkubwa kwao.
Katika halmashauri ya wilaya ya Njombe zoezi hilo
limeanza katika kata na vijiji mbalimbali ambapo wakazi wa kijiji cha Ikuna
baadhi ya walengwa hao akiwemo John Kipapi
na Sesilia Wudumbe wamesema fedha ambazo wamekuwa wakizipata zimekuwa
zikiwasaidia katika kukidhi mahitaji mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto,kufuga
na hata kujenga licha ya kuiomba serikali iwaongezee kiwango cha fedha kama
inawezekana.
“Mradi huu kwa kweli ni mzuri lakini kwa kuwa
wengine ni fukara wakubwa basi ingeongezwa kidogo mpaka hamsini elfu ingesaidia
sana,nah ii inasaidia kununua mbolea hata shughuli nyingine ndogo ndoo”alisema
John Kipapi
Kenan Ngimbudzi ni mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ikuna
ambaye anatoa ushauri kwa serikali juu ya mabadiliko ya mfumo wa upokeaji fedha
hizo ambazo kwa sasa zitaanza kutolewa njia ya benki au simu tofauti na hapo
awali.
“Swala zima ni kuwaambia wanaowahudumia walengwa
wasifanye hujuma,lakini kwa njia ya simu ukiangalila zoezi litarudi lile la
makato na tutarudi kulele wakati fedha yenyewe bado ni ndogo,kwa hiyo swala la
kuibiwa kwa walengwa naona litakuwa kama awali ambavyo wasaidizi wa kaya walikuwa labda wanakabidhiwa”alisema
Kenan Ngimbudzi
Kwa upande wake mwezeshaji wa TASAF ngazi ya halmashauri bwana Godfrey Kitulama ameeleza
namna zoezi lilivyokwenda na kwamba kumekuwapo na baadhi ya changamoto zikiwemo
za baadhi ya wazee kusahau nyaraka muhimu kama vitambulisho vya nida na mpiga
kura hatua ambayo imekuwa ikichelewa zoezi la kuhakiki.
“Zoezi linaendelea isipokuwa changamoto kubwa ni
wanufaika wa TASAF wengine hawana
vitambulisho vya NIDA na wengine vya wapiga Kura lakini wenye navyo tunaweza
kuwasajili na ambao hawana wamendelea kutafuta viambata hivyo na kinachosababisha
walio wengi ni wazee ndio maana uelewa uko tofauti na wanakuja bila
vitambulisho”alisema Godfrey Kitulama
Mradi wa TASAF katika kipindi hiki cha pili awamu ya tatu
umeanza kwa kufanya uhakiki wa walengwa sahihi ili kuwaondoa watu hewa
wanaonufaika kinyume cha taratibu.
0 Comments