Na Amiri Kilgalila,Njombe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema mkoa wa Njombe Rose Mayemba,amesema chama hicho kimejipanga kuweka
wagombea wa ubunge katika majimbo yote
ya uchaguzi mkoani Njombe
Rose
ameyasema hayo mkoani Njombe wakati wa mahojiano na kituo cha Radio King’s
kilichopo halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo
“Wananchi wajitokeze kuwasikiliza pale ambapo
tutakuwa tumeanza mtanange,tunawagombea
katika majimbo yetu yote sita na
ni wagombea wazuru tunaamini mambo yatakuwa mazuri” Rose Mayemba Mwenyekiti
Chadema Njombe
Vile vile Rose amesema
“Chadema mkoa wa Njombe tumejiandaa na tunawagombea
wa kutosha,tuna kata 107 lakini tunawagombea karibu kila na ni mkakati kwamba
hakuna kata itakwenda kwenye uchaguzi bila kuwa na mgombea” Rose Mayemba
Mwenyekiti Chadema Njombe
0 Comments