TANGAZA NASI

header ads

CHADEMA Njombe washangaa wabunge wasio jua pesa zao za michango zinakoenda



Na Amiri Kilgalila,Njombe

Uongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Njombe kupitia kwa mwenyekiti wake Rose Mayemba umeshangazwa na kitendo cha wabunge ambao hivi karibuni wamekuwa wakihama chama hicho na kutoa hoja za kushindwa kuelewa matumizi sahihi ya michango yao kama wabunge.

Rose akiwa katika  moja ya kipindi  cha Radio King’s fm kilichopo Njombe mjini amenukuliwa akisema kuwa

“Mfamaji haishi kutapatapa,kwasababu ni hatari ukiona Mbunge ambaye uliaminiwa halafu unatoa pesa ambayo hufahamu inakoenda ni hatari,ninachoweza kusema hakuna jambo ambalo linafanywa nje ya misingi ya katiba yetu”Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe
Kuhusu Chama hicho kukaguliwa Bi,Rose alisema

“Chadema ni Chama cha kisiasa ambacho kinakaguliwa na mdhibiti na mkaguzi wa mahesabau ya serikali,fedha yote inayokatwa kwa wabunge wetu Bunge linafahamu na hii si Chadema peke yake hata CCM wana utaratibu wao wa kukusanya fedha kwa wabunge” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

Vile vile ameongeza kuwa katikka kipindi cha miaka mitano fedha nyingi zilitumika katika zoezi la Chadema Msingi

“Tulikuwa na zoezi la Chadema ni msingi Nchi nzima kwa miaka mitano ambapo tulizuiliwa siasa za majukwaa,watu wametumwa maeneo mbali mbali na ndio maana Chadema ipo kwenye kila kitongoji na zimetumika Milions” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

Aidha amesema michango ya wabunge na mingine pia imesaidia na kuwezesha ongezeko la wanachama wa chama hicho

“Chadema sasa hivi ina wanachama zaidi ya milioni 10,na wamepatikana kwasababu ya michango ya wabunge,michango ya wadau ikiwa ni pamoja na ruzuku tunayoipata kutoka serikalini” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

 “Hizi piki piki za Chama M4C kutoka kiwandani zimenunuliwa si kwa fedha ya kwenye mfuko wa mwenyekiti ni kutokana na michango ya wanachama,wabunge,wadau pamoja na ruzuku kutoka serikalini” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

 “Nafikiri mmekuwa mkiziona barabarani,na hizi gari zote hazijatoka na mwenyekiti wa chama,zimetokana na michango ya wadau,kadi za wanachama,michango ya wabunge na ruzuku ya serikali” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

Hata hivyo amesema inastaajabisha kwa wabunge wanaotoka ndani ya chama hicho kuhoji matumizi ya pesa wakati shughuli za chama zinaendelea majimboni mwao

“Sasa ni jambo linalostaajabisha kidogo mbunge kuhoji matumizi ya fedha aliyoitoa wakati yeye akiwa bungeni Dodoma kuna watu wako jimboni kwake usiku na mchana wanafanya kazi ya ujenzi wa Chama” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

 “Mbunge anayehoji fedha inakokwenda wakati anatazama kwa macho yake fedha inakoenda huyo ana lengo lingine  zaidi ya kuhoji,wanakuwa na ajenda za sili zaidi ya fedha wanayohoji kwasababu fedha inaonekana na wananchi wanaona ni namna gani inatumika” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe

Post a Comment

0 Comments