TANGAZA NASI

header ads

TAKUKURU yaokoa zaidi ya milioni 219 Kagera


Na Clavery Christian, Bukoba Kagera.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Kagera imefanikiwa kuokoa kiasi cha fedha sh, milioni mia mbili kumi na tisa laki saba hamsini na nane elfu na mia tisa thelathini na saba na senti tisini na nane pamoja na jenereta na mtungi mmoja wa gesi, blenda ya kusagia juisi na jiko la gesi lenye plet mbili vyote vikiwa na thaman ya shilingi laki 665, 000 vilivyokuwa vimechukuliwa na mkopeshaji wa mikopo umiza aliyekuwa amekopesha jumla ya shilingi laki moja na nusu tu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa Takukuru mkoani Kagera bw, John Joseph amesema kuwa milioni 57 zinatokana na ukwepaji wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara wawili ambapo kila mmoja alikwepa kulipa kodi kwenye mamlaka ya mapato Tanzania TRA na mwingine kwa kamishina wa madini.

Aidha kiasi kingine cha fedha kimetoka kwenye kampuni ya ujenzi wa barabara iliyokwepa kulipa kodi ya madini ujenzi kwa afisa madini mkoani Kagera kutokana na kutumia madini ujenzi katika shughuli zake

Pamoja na fedha hizo kurejeshwa pia kiasi cha shilingi milioni arobaini na nne laki tisa na elfu arobaini na mbili ni fedha ambazo fedha zilizorejeshwa kwa wananchi mbalimbali kutokana na mikpo umiza ambao walikuwa wamekopa kwa wakopeshaji.

Kiasi kingie cha fedha shilingi milioni 42,956,,180/= zimerejeshwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Biharamulo kutokana na ubadhilifu wa makusanyo ya ndani POS, Huku shilingi milioni 25,826,661/= ni fedha zilizorejeshwa kutoka kwa wadaiwa sugu wa sukari Saccos iliyoko katika kiwanda cha Kagera Suger wakati kiasi cha shilingi milion 22,233,622/46 ni fedha za zilizorejeshwa kutoka kwa wadaiwa Sugu wa banki ya wakulima KAGERA FARMERS COOPERATIVE BANK (KFCB).

Post a Comment

0 Comments