Na Jackline Victory,Dodoma
Mkurungezi mtendaji
wa taasisi ya chakula na lishe TFNC Dkt,Germana Leyna amesema hayo ni kwa mujibu
wa kiwango cha kimataifa. Kuwa ili jamii isiwe na matatizo ya ambayo yanatokana
na upungufu wa madini joto
Leyna amesisitiza kuwa jamii kuona umuhimu wa
kutumia chumvi yenye madini joto ambayo ni tosheleza hasa watoto wadogo
kwaajili ya ukuaji wa ubongo
“Toka mwaka 2015 kiwango cha kaya ambazo kinatumia
chumvi yenye madini joto ya kutosha hakijaongezeka,kimebakia pale pale kwenye
asilimia 60% kwa hiyo tumekuwa tukijaribu kutafuta ni sababu gani ambazo
zinasababisha ni sababu gani ambazo zinasababisha idadi ya kawa ambazo
zinatumia madini joto toshelevu”alisema Dkt,Germana Leyna
Anna John ni afisa lishe mwandamizi kutoka
Taasisi ya chakula na lishe Tanzania amesema upungufu wa madini joto bado
ni changamoto na huathiri watu wa makundi yote.
“Upungufu wa madini joto ni tatizo kubwa na tatizo hili huwaathiri sana
watu wa makundi yote na kirubishi hiki cha madini joto kinapatikana ardhini ila
kwasababu ya mafuriko na matatizo mengine ya mabadiliko ya tabia ya nchi
utakuta kwenye ardhi tena kirutubisho hiki hakipatikani kwa urais.Kwa hiyo
mwanadamu anaweza akapata madini joto kwa kula vyakula ambavyo vimepandwa
kwenye ardhi yenye madini joto ya kutosha”alisema Anna John
Tanzania
imetajwa kutopanda katika Kiwango cha kaya zinazotumia chumvi yenye
madini joto ya kutosha na kuendelea kusalia na asilimia 60 kutoka
mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020.
Hatahivyo, Kirutubishi cha madini joto kinapatikana
ardhini lakini kutokana na mabadiliko ya tabia Nchi pamoja na mafuriko ambayo
yanatokea yamechangia kuondoka na udongo wa juu wa madini joto.
0 Comments