TANGAZA NASI

header ads

Zanzibar joto lazidi kupanda,wengine wawili wachukua fomu ya Urais




Na Thabit Madai,Zanzibar

ZOEZI la uchukuaji wa Fomu za kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, lazidi kupamba moto ambapo Mohamed Hija Mohamed na Balozi Meja Jeneral Mstaafu Issa Suleimani Nassor wamefika Ofisini hapo kisiwandui kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo.

Wa kwanza kati ya hao kufika ofisini hapo alikuwa Mohamed Hijja Mohamed ambapo  aliwasijili majira ya saa saba nusu Ofisini hapo na kukabidhiwa fomu na Katibu wa Kamati Maalumu  ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Mohamed hija Mohamed aliwashukuru Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa waayoifanya ya kuwahabarisha wananchi juu ya zoezi zima la uchukuaji fomu linaloendelea.

Pia alipongeza chama chake cha mapinduzi kwa kuandaa utaratibu mzuri kwa wanaokuja kuchukua fomu ya kuwani nafasi ya urais wanapata fursa ya kuongea na waandishi wa habari sambamba na mapokezi mazuri.

“Kwanza niwapongeze chama changu kwa zoezi hili na mimi Mohamed Hijja Mohmed nimechomoza kugombania nafasi hii ya urais kwa ridhaa ya chama changu,nami naungana na wenzangu kuwa leo nimechukua karatasi hizi chama change kikinipa ridhaa tutazungumza mengi”  alisema Mohamed Hija Mohamed.


Wa pili kufika ofisini hapo alikuw Balozi Meja Jeneral Mstaafu Issa Suleimani Nassor na kukabidhiwa fomu na Katibu wa Kamati Maalumu  ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu Balozi Meja Jeneral Mstaafu Issa Suleimani aliahidi kwamba endapo chama cha Mapinduzi CCM kitampa ridhaa ya kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho ataendeleza yale yote mazuri yaliofanywa na uonhozi uliopita na kuahidi kukuza uchumi wa Zanzibar.

Hadi sasa jumla ya Wanchama wa chama hicho Tisa   tayari waeshajitokeza kuchukuaafomu yakuwania nafasi hiyo ya Urais ambao wa kwanza kufungua pazia
alikuwa ,Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Karume, Mbwana Yahaya Mwinyi,
Omari Sheha Mussa na Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi, Shamsi Vuai Nahodha na Mohamed Jaffar Jumanne, Mohamed Hijja Mohamed na Balozi Meja Jeneral Mstaafu Issa Suleimani.



Post a Comment

0 Comments