Na Amiri kilagalila,Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Chiristopher Ole Sendeka,amepokea
msaada wa fedha shilingi milioni mbili zilizotolewa na ujumbe wa viongozi wa
dini wa kanisa la Tanzania assemblies of God (TAG) jimbo la Njombe kusini,
uliongozwa na askofu wa jimbo hilo, Phairod Nyagawa kwa ajili ya kusaidia kukabiliana
na virusi vya Corona.
“Kwa hiyo nalipongeza kanisa kwa kumuunga mkono
Mh.Rais katika msimamo aliouchukuwa”alisema Ole Sendeka mara baaa ya kukabiiwa
fedha
Vile vile Kufuatia agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli
kutaka shule zote za msingi na sekondari zifunguliwe juni 29, mwaka huu, mkuu
wa mkoa wa Njombe, Christoipher Ole Sendeka ameagiza shule za msingi na
sekondari zihakikishe zinaendelea kuwa na kamati ndogo za afya
zitakazohakikisha zinachukua hatua stahiki ya kusimamia wanafunzi wanazingatia
ushauri wa wataalam wa afya wa kujikinga na ugonjwa CORONA
“Tupokwenda kufungua shule nachukuwa nafasi hii
kuwaagiza wakuu wa wilaya,na wakurugenzi pamoja na waganga katika halmashauri
zetu,kuhakikisha kila shule na taasisi za elimu ziendelee kuwa na kamati ndogo
za afya zitakazokuwa zinatoa elimu kwa faia ya vijana wetu”alisema Sendeka
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Njombe, amelishukuru
kanisa la TAG mkoa wa Njombe kwa dhamira yao ya dhati waliyoionyesha ya kuunga
mkono juhudi za serikali za kukabiliana na janga hilo
Naye askofu
wa kanisa la TAG jimbo la Njombe kusini Phairod Nyagawa ameipongeza na kuiunga
mkono serikali kuhusu mikakati iliyowekwa ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa
wa corona,bila kuathiri shughuli za kiuchumi za wananchi.
“Jimbo la Njombe kusini tunaungana na serikali kwa
kutoa shilingi milioni mbili ili uongozi wa mkoa uangalie namna unavyoweza kuhakikisha
unasaidia katika mapambano dhii ya Covid-19”alisema Phairod Nyagawa askofu wa kanisa la TAG jimbo
la njombe kusini
Kutolewa kwa msaada huo ni hatua mojawapo ya
mwitikio chanya wa mashirika na taasisi za kidini mkoani Njombe kujitokeza kutoa
msaada wa hali na mali,lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika
kupambana na CORONA
0 Comments