Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wananchi wa kitongoji cha Mking’ino kijiji cha Luvuyo
kata ya Madope wilayani Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kuboresha
miundombinu ya barabara inayounganisha kijiji chao na vijiji jirani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma
mbalimbali za kijamii.
Wakazi hao akiwemo Erasto Mtega, Junitha Mbukwa na Stia
Chaula wamesema asilimia kubwa ya wakazi wa eneo hilo ni wakulima wa mazao ya
viazi mviringo na mahindi lakini changamoto ya ubovu wa barabara inawalazimu
kuuza mazao yao kwa bei ya chini tofauti na maeneo mengine.
“Mfano muda wa masika tunapata tabu sana kwenye
usafirishaji,tunweza tukalima mahindi lakini yanaozea shambani kwa kushindwa
kusafirisha,tunaomba Mh,Rais aangalie
kwa jicho lingine”alisema Stia Chaula
Aidha wamesema licha ya kuwa jirani na kata za Lupanga
na Mlangali zilizopo wilayani Ludewa lakini kitongoji cha Mking’ino hakina
barabara ya uhakika inayoelekea kwenye maeneo hayo jambo ambalo limekuwa
likisababisha wakazi wa eneo hilo wakiwemo akina mama na watoto kupata shida ya
kufuata huduma za afya pindi wanapo ugua.
Licha ya kukiri uwepo wa changamoto ya ubovu wa
barabara katika baadhi ya maeneo ya kata ya Madope diwani mstaafu wa kata
hiyo Policap Mlelwa amesema serikali
kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini tarura wilayani Ludewa imeanza
kuboresha baadhi ya barabara hizo ikiwemo ya kutoka kijiji cha Madope kuelekea Luvuyo.
“Ninahakika kwamba wananchi wangu wa Mking’ino
wanachangamoto ya barabara,lakini kwa mara ya kwanza tumeifikisha eneo Fulani
kwa kutengeneza kwa gleda ila kwasababu ya mvua ile barabara bado ni
mbaya,lakini kwasababu fedha tuliyoipata inaishia inaishia Luvuyo ninaimani
20/21 tutakwenda mpaka Mking’ino na barabara ile tumeijenga KM 3 kwa kokoto
lakini inaendelea kuboreshwa”alisema Mlelwa
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Pombe
Magufuli imejipambanua wazi katika kufanyakazi ikiwemo kuelekeza nguvu kubwa
katika sekta ya miundombinu lakini wakazi hao bado wanalia na changamoto ya
barabara.
0 Comments