TANGAZA NASI

header ads

Wadau wa kituo cha mabasi Makambako walalamika kwa kushindwa kuondolewa kifusi ndani ya kituo

Picha ni banda la kupumzika Abiria

Na,Clief Mlelwa

Wadau wa kituo kikuu cha mabasi mjini Makambako mkoani Njombe wameiomba serikali ya halmashauri hiyo isambaze kifusi ambacho kimemwagwa ndani za kituo hicho bila kutawanywa kwa muda wa wiki mbili sasa.

Wakizungumza na kituo hiki  wamesema kuwa kutokana na kifusi hicho kukaa kwa muda wa wiki mbili bila kusambazwa kimesababisha adha kubwa wa watumiaji wa kituo ikiwemo vumbi na kunusurika kugongwa na magari.

Aidha mwenyekiti wa kituo ABUSALUM MAGOMA amesema kuwa kutokana na adha hiyo wameshawasilina na halmashauri na wameahidi kuifanyia kazi mapema ili kuondoa adha hiyo.

Nae meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA katika halmashauri ya mji wa Makambako Mhandisi ANYETIKE KASONGO amesema kuwa kifusi hicho kitasambazwa ndani ya wiki hii.

Post a Comment

0 Comments