Na John Claud
Jeshi la polisi mkoani Morogoro
limefungua kituo cha polisi Mbingu kilichopo wilaya ya kilombero baada ya
wananchi kujichukulia sheria mikononi kukichoma moto mwaka 2015 wakitaka
kufanya jaribio la kumua mtuhumiwa aliefikishwa kituoni hapo na kisha
jeshi hilo kufanikiwa kumtorosha.
Akizungumza na wananchi wa kijiji
hicho kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Willbroad
Mutafungwa amesema kuwa ameridhishwa na ujenzi wa kituo hicho licha ya
kutokukamilika kwa asilimia zote na sasa ni wakati muafaka wananchi
wa kijiji hicho kupata huduma za kipolisi huku mambo mengine yakiendelea
kukamilishwa.
Katika hatua nyingine Kamanda
Mutafungwa amewataka wenyeviti wa vijiji wilayani kilombero kuweka
utaratibu wa kuanzisha kamati za ulinzi na usalama zitakazo wachagua
vijana walio waadilifu ambao watakuwa ni sehemu ya ulinzi
shirikishi na polisi jamii ili kuimarisha doria sehemu mbalimbali
za maeneo yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji
cha Mbingu Erasto Mgenda amelishukuru jeshi la polisi kwa kukubali
kuzindua kituo hicho kipya huku akiliomba kuwapatia askari waaminifu ambao
watashirikiana na wananchi wa kijiji hicho.
Bahati Mwakagugu ni mkazi wa kijiji cha Igima amesema
kuwa kwa muda wa mika mitano wamekuwa wakilazimika kutumia gharama kubwa
kusafiri umbali mrefu hadi kijiji jirani ili kupata huduma za kipolisi
hasa yanapotokea matukio ya kihalifu.


0 Comments