Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Ibumi Tarafa ya Liganga Wilayani Ludewa Mkaoni Njombe imesema haitasita kuwakamata na kuwashughulikia kisheria wale wote wanaojihusisha na masuala ya kisiasa kabla ya muda uliopangwa kuanza shuhuli za uchaguzi.
Akitoa
Taarifa yenye tahadhari mbele ya wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata
Ibumi Afisa mtendaji huyo wa kata Bw,Felix Charle viongozi waliochaguliwa mwaka 2015 na kupewa
dhamana ya kuongoza bado wanafanya kazi hivyo atakaye onekana anafanya kampeni
zinazohusu uchaguzi atakamatwa.
Katika hatua nyingine Bw,Charle ameongeza kuwa ni kosa la jinai mtu
kufanya siasa kabla ya wakati
kufika au Mamlaka husika hazijatoa maelekezo kwani kufanya hivyo kuikosea
sheria ya uchaguzi.
Afisa Mtendaji huyo ametoa wito kwa kuwataka
watanzania waendelee kufanya shughuli za kimaendeleo ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja,familia na Taifa


0 Comments