SERIKALI
imekamilisha azma ya kuwa na benki moja mahsusi
ya biashara baada ya kuunganisha benki
zake mbili za biashara,benki ya Uwekezaji Tanzania(TIB Corporate Limited) na
benki ya Posta Tanzania(TPB blank Plc).
Lengo la
kufanya hivyo ni kuifanya benki kuwa imara,kuongeza ufanisi na kupunguza
gharama za uendeshaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dodoma,Msajili wa hazina Athuman Mbutuka
amesema muunganiko huo ni hatua mojawapo inayochukua zenye lengo la kuboresha
utendaji wa mashirika na taasisi za umma.
Mbutuka
amewahakikishia watanzania kuwa muunganiko huo hautaathiri huduma za kibenki.
Mei 26
mwaka huu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango aliweka bayana dhamira
ya kuunganisha mifuko hiyo wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa wakati wa
mjadala wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali(PAC)kuhusu taarifa
za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG)zilizokaguliwa na
serikali kuu na mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha unaoishia mwezi juni 2020.
Pamoja na
muunganiko huo serikali imewahakikishia wafanyakazi waliokuwa katika benki hizo
kuwa ajira zao hazitaathirika.


0 Comments