TANGAZA NASI

header ads

Polisi Arusha yasambaratisha ndoa ya mwanafunzi wa shule ya msingi


Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limefanikiwa kuzima jaribio la mwanafunzi wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 12,aliyetaka kuozeshwa na wazazi wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna,alisema wanashikilia watu wawili akiwemo baba mzazi wa binti huyo, Saiboka Memriki na mwanaume aliyetaka kumuoa binti ambaye ana umri wa miaka 45.

Alisema siku za hivi karibuni, kumeibuka wimbi la baadhi ya wazazi wenye tamaa ya fedha na mifugo kuozesha watoto wao ambao ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao wako majumbani kutokana na ugonjwa wa corona.

Alisema tukio hilo, lilitokea Kata ya Musa wilayani Arumeru,ambapo kabla hawajafanikisha mpango wa kumuozesha mwanafunzi, polisi kwa kushirikiana na wananchi walitoa taarifa.

“Hivi karibuni kuna wimbi limeibuka la watu hususani wenye tamaa ya mahari katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wako nyumbani kutokana na corona kutumia nafasi hiyo kuozesha wanafunzi” RPC Arusha

“Huko Kata ya Musa wazazi walitaka kumwozesha mtoto wao kwa mwanaume, kabla hawajafanikisha nia yao hiyo ovu, jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kudhibiti tukio na kukamata na baba mzazi na mwanaume aliyetaka kumuoa mwanafunzi huyo” RPC Arusha

Post a Comment

0 Comments