TANGAZA NASI

header ads

Nahodha wa Lipuli na wenzake 3 hawajafika mazoezi




NZEYIMANA Mailo, Kocha Mkuu wa Lipuli amesema kuwa wachezaji wake wanne hawajaanza mazoezi pamoja na timu kwa sasa.

Lipuli FC yenye maskani yake Iringa ilianza mazoezi, Mei 31 Uwanja wa Samora kwa ajili ya kujiaanda na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

 Mailo amesema kuwa:“Wachezaji wanne hawapo mazoezini ambao ni Paul Nonga, David Mwassa,Seif Karihe na Daruesh Saliboko."

Paul Nonga ambaye ni nahodha wa Lipuli amesema kuwa kuna mambo anashughulikia kabla ya kuibuka kambini.

Post a Comment

0 Comments