Rais
wa kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuendelea kufungwa kwa shule zote pamoja na vyuo vikuu
nchini humo hadi Septemba Mosi mwaka huu ambapo vitafunguliwa tena.
Akilihutubia
taifa hilo kutoka ikulu ya rais jijini Nairobi Kenyatta amesema kuwa
amechukua hatua hiyo ili kulinda maisha ya wanafunzi na walimu haswa
kutokana na idadi kubwa ya maambukizi ya virus vya corona yanayo kuwa kwa kasi katika nchi hiyo.
Aidha ametangaza kuongezwa kwa muda wa marufuku ya
kutoka nje kwa mwezi mmoja zaidi amri iliyotangazwa na serikali
kudhibiti maambukizi ya Corona ila muda wa utekelezwaji wake
ukibadilishwa na kuanza saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri.
0 Comments