Mkuu
wa Mkoa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti ametoa siku 7 kwa
watumishi wa halmashauri ya wilaya Biharamulo waliokusanya fedha na
kushindwa kuzipeleka Banki wawe wamezipeleka ndani ya siku saba.
Gaguti
ametoa agizo hilo wakati wakikao cha baraza la madiwani wa halmashauri
hiyo lililolenga kujibu hoja za mthibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG
ambazo miongoni mwa hizo ni makusanyo ya fedha Zaidi ya shilingi milioni
224 ambazo hazikupelekwa bank.
“CAG
ametoa hoja mbalimbali kuhusu halmashauri hiyo na nyingi zinalalia
masuala ya fedha, natoa siku saba kwa watendaji ambao wamehusika na
kutopelekwa fedha hizi wawe wamezirejesha mara moja na kwenye hili
sitanii kabisa tutakuja kuonana wabaya kwenye fedha za umma.” Amesema
Gaguti.
Mkuu huyo amemuomba mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuitisha kikao kingine maalumu
ambacho kitakuwa na agenda za kuangalia mwenendo mzima wa watumishi
ndani ya halmashauri hiyo ili hatua husika ziweze kuchukuliwa pale
itakapostahili.
katika hatua nyingine madiwani wakichangia kwa nyakati tofauti kwenye hoja za hizo za CAG
wameitaka halmashauri kumalizia miradi mbalimbali ambayo wananchi
tayari wameshaweka nguvu zao hasa vumba vya madarasa ili kusaidia watoto
kusomea katika mazingira ambayo ni mazuri na salama kwaajili ya maisha
yao ya baadae.
Madiwani
hao wamesama kuwa halmashauri hiyo inatatizo la uhaba wa watendaji
Zaidi ya 30 wa vijiji suala linalopelekea ukusanyaji wa mapato kuwa
hafifu kwakuwa wanaopewa jukumu la kukusanya wengi wao hawana elimu juu
ya mashine za pos zinazotumika kukusanyia mapato na kufanya kuwa
changamoto ya kudumu.
Halmashauri
ya wilaya Biharamulo ni miongoni mwa halmashauri 8 zinazouunda mkoa wa
Kagera ambayo kwa kipindi cha miaka minne mfurulizo imepata hati safi
licha ya kuwa na changamoto ya kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato ya
ndani hali ambayo mkuu wa mkoa ameagiza ishugulikiwae mara moja.
0 Comments