TANGAZA NASI

header ads

MAKAMBAKO:WATISHIA KUTO LIPA USHURU WA KITUO CHA MABASI




Na Clief Mlelwa, Makambako

Wadau wa stendi kuu ya mabasi mjini Makambako,mkoani Njombe wametishia kutolipa ushuru wa standi hiyo mpaka pale kifusi ambacho kimemwagwa zaidi ya wiki tatu kitaposambazwa.

Wadau wa stendi hiyo wakiwemo madereva na maafisa usafirishaji wamesema kuwa kutokana na stendi hiyo kutokufanyiwa marekebisho imepelekea magari yao kuharibika mara kwa mara

Naye mwenyekiti wa stendi hiyo ABUSALUM MAGOMA amesema kuwa anashanganzwa na serikali kushindwa kusambaza kifusi hicho licha kuahidi kufanyia kazi wiki iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) katika halmashauri ya mji wa Makambako mhandisi ANYETIKE KASONGO amesema kuwa kifusi hicho kitasambazwa hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments