Na Ignatio Cherls,Ludewa
Kijana anayefahamika kwa jina la
Chesco Mtega mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kitongoji cha Kanisa A Kijiji cha
Ludewa,wilayani Ludewa mkoani Njombe amegundulika amejinyonga kwa kutumia shuka
lililofungwa juu ya kenchi na shingoni mwake ndani ya nyumba,huku sababu
zikitajwa ni kutokana na msongo wa mawazo (SONONA)
Akizungumza na waandishi wa habari
akiwa ofisini kwake mkuu wa Wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama wilayani humo Mh, Andrea Tsere amesema inadaiwa kijana
huyo alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo.
“Inadaiwa huyu kijana alifanya
hivyo kwasababu ya msongo wa mawazo,sijajua alikuwa na historia gani lakini pia
inaonekana alikuwa mtundu mtindu zaidi” Alisema Tsere
“Tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi
ni kwanini hasa amefikia hatua ya kujinyonga,historia yake ikoje,ndugu zake wanaushirikiano
gani,anadaiwa nini,kuna mgogoro gani kwenye familia,kwasababu mtu mzima mpaka
anafikia hatua ya kujinyonga lazima kuna jambo ndani yake”aliongeza Tsere
Aidha Tsere ametoa wito kwa wananchi
kushirikiana na ndugu wa karibu katika mawazo au changamoto ili kutatauliwa
badala ya kukaa kimya na kusababisha matatizo.
“Wito wangu kwa makabila yote ni
kuwasihi watu wote wajaribu kushirikiana na ndugu zao,wakubwa zao,wadogo zao
katika changamoto walizo nazo ili waweze kutatua badala ya kukaa nazo na
baadaye unajinyonga”aliongeza Andrea Tsere
Vile vile ametaka watu kumuomba
Mungu atakayeweza kuonyesha njia kwasababu watu wanaofikia hatua ya kujitoa
uhai wanakuwa wamejitenga na Mungu kwa muda mrefu.
0 Comments